Saturday, 1 February 2014

MWANAFUNZI AMKA MAPEMA UWAHI USAFIRI,MZAZI MSAIDIE MWANAO!.

Ukimuuliza mwanafunzi yeyote anayetumia usafiri wa umma kwenda shuleni asubuhi, ni changamoto gani anazozipata wakati anakwenda na kurudi shule, tatizo la usafiri basi litakuwa ni miongoni mwa matatizo atakayokwambia.

Wanafunzi wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa ya usafiri aswa kwa wale waishio katika jiji la Dar es Salaam ambapo tatizo hili limekuwa dondandugu na ni sababu kubwa ya wao kuchelewa kufika shule na wengine kurudia njiani.

Tatizo hili usababisha wanafunzi kukosa baadhi ya vipindi ambavyo kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya mchango katika ufaulu wao, hivyo, wanapokosa vipindi hivyo inawawekea nafasi kubwa ya kufanya vibaya kwenye masomo yao.

Ili kuwawezesha wanafunzi kuwahi shule wanafunzi wanashauliwa kuamka mapema ili wawai usafiri utakaowawezesha kufika mapema na kuwai vipindi vya asubuhi.

Zoezi hili la kuamka mapema, mzazi pia anashauliwa kuwasaidia watoto wao kuwaimiza watoto wao kuamka mapema ili kuepusha matatizo yanayoweza kujitokeza.

Mzazi ana jukumu la kumsimamia mtoto pale panapohitajika kusaidiwa, mzazi ana wajibu wa kuhakikisha mwanae anaamka mapema ili kuwahi shule.

Tatizo hili la usafiri kwa wanafunzi kwa namna moja ama nyongine limekuwa likiwaathili sana kisaikologia ambapo baadhi ya wanafunzi wamejikuta wakijiingiza katika vitendo viovu vya kulumbana na makonda.