Saturday, 1 February 2014

MUME ATUHUMIWA KUIBA BIDHAA ZA BIASHARA.

Dada mmoja mkazi wa Kiwalani Dar es salaam ambaye hakutaka  jina lake litajwe amejikuta akiingia kwenye harakati za kumtafuta mumewe anayemshtumu kwa kosa la kumuibia bidhaa zake za biashara ndogondogo.

Dada huyo anayeendesha shughuli zake za kijasilia mali alisema kwamba tabia ya mume wake kumwibia bidhaa za biashara yake ni ya tangu muda mrefu na amekuwa akimtia harasa mara kwa mara.

"Ananitia hasara sana, nashimdwa kuendelea mbele kwa sababu yake, kama jana nilienda mjini kukunua katoni ya majani ya chai yeye alipokuja akaondoka nalo. Sasa jamani si hasara hii?", alilalamika dada huyo.

Dada huyo aliongezea kwamba anahisi mume wake anaiba bidhaa hizo na kuzipeleka nyumba ndogo.

Juhudi za kumtafuta mume huyo kwa ushirikiano na mke ili aweze kujibu tuhuma hizo hazikuweza kufanikiwa.