Baada ya Mwana FA kutuambia bado yupo yupo sana kwenye maisha ya kibachela sasa ameamua kuachana na hayo na kuamua kufunga pingu za maisha.
Rapa Mwana FA amefunga ndoa Jumapili hii ‘June 5 2016’ na mchumba wake Helga ambaye pia na mama wa mtoto wake.
Kufuatia tukio hilo mwanamuziki wa Bongo fleva Ommy Dimpoz hakusika kutoa pongezi zake kwa Mwana FA na kumpatia baraka zote katika ndoa yake na Bi Helga.
Dimpoz ameandika haya katika Instagram,
"Congratulation the hip hop Billionare kwa kuuaga ukapera mwenyezi Mungu awajaalie maisha mema na yenye baraka we na bi Helga mzikane inshallah."