Familia ya wasafi inayoongozwa na Diamond Plutinumz mapema leo ilifanya ziara ya kwenda ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakiwa na lengo la kuchangia madawati lengo ambalo limetimia kwa familia hiyo kuchangia madawati 600 kwa ajili ya shule za mkoa huo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mkubwa wa wasafi, Diamond ameeleza kuwa madawati hayo yataweza kuwasaidia wanafunzi 1,800 ambao hawataweza kukaa chini tena na badala yake kukaa sehemu nzuri na kupata elimu safi.
Pia katika ukurasa wa Wcb wasafi wameposti taarifa inayozungumzia mkuu wa wa mkoa wa Dar Paul Makonda kutoa shukrani zao kwa mkuu huyo ambaye amejitole kuwa mlezi wa familia ya wasaifi.
Diamond akiwa ofisini kwa Makonda.