Ulishawahi kufikiria ni kwa kiasi gani ufanyaji wa
mapenzi kinyume na maumbile unaweza kumwathiri mtoto wa kike? Ni kitendo
kinachoweza kusababisha kifo kwa mlengwa.
Ni mama wa makamo aliyekutwa akimsimulia mwenzie
kile kilichomkuta mjukuu wake aliyekuwa akifanya mapenzi kinyume na maumbile na
mume wake kwa muda mrefu.
Mama huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema
kuwa mjukuu wake huyo alikuwa na mazoea ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na
mume wake.
Alianza kufanya tendo hilo tangu muda mrefu kiasi
kwamba tabia hiyo ilijenga mazoea na kuwa mchezo ambao hakuweza kuuacha.
Ilifikia kipindi yeye na mume wake waepuka kupata
ujauzito wakihofia kupata shida wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa
mama wa mjukuu huyo, wakati wa uhai wake, mjukuu huyo alishatoa mimba karibia
sita akishirikiana na mume wake.
Siku za mwizi ni harobaini, kwenye chezacheza yao
ujauzito ukapatikana. Bila shaka mchakato wa kuichoropoa ulishindikana na
kuamua kuiacha.
Wakati wa kujifungua ulipofika, mjukuu huyo
alishikwa na uchungu na kupelekwa hospitali tayali kwa kujifungua.
Inasemwa kwamba wakati wa kujifungua, njia sahihi
ambayo mtoto alitakiwa apitie ikagoma kufunguka. Cha ajabu njia ya haja kubwa
ndio iliyokuwa inafunguka.
Baada ya kufahamu nini kinaendelea madaktari
waliokuwa wanamhudumia mjukuu walishauli kuwa anatakiwa afanyiwe upasuaji kwa
kuwa mjukuu huyo hawezi kujifungua kwa njia ya kawaida.
Ndugu wa mjukuu walijulishwa na kukubaliana na
ufanywaji wa upasuaji ili kuokoa maisha ya mtoto wao.
Baada ya upasuaji, mjukuu alirudi nyumbani na mtoto
wake huku akiwa na kibarua cha kuuguza kidonda cha upasuaji.
Baada ya siku kadhaa baadae, mjukuu alianza
kuharisha mfululizo chanzo kikiwa ni njia yake ya haja kubwa kulegea kutokana
na ufanyaji wa mapenzi kinyume na maumbile.
Siku kadhaa baadae mjukuu alizidiwa na homa na
kufariki dunia na kuacha mtoto wa miezi kadhaa.