Ilidhaniwa kuwa ukuaji wa teknolojia ungeweza kuleta
mabadiliko chanya kwenye sekta ya habari lakini badala yake teknologia hii
inageuzwa kuwa chanzo cha kuichafua sekta ya habari kwa baadhi ya watu
kuchapisha na kusambaza picha na video za ngongo kwenye mitandao ya kijamii kwa
kutumia blog.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la
mabloga wanaojihusisha na uchapishaji wa picha na video za ngono suala ambalo
linadhalilisha tasnia ya habari.
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii haswa Facebook
kumekuwa kimbilio la mabloga wengi wanaochapisha picha na video za ngono katika
blog zao na kuzituma mtandao.
Watu hawa wachache wanaotumia blog zao kuchapisha
picha zisizo na maadili kwa jamii wanapelekea mabloga wengine wasafi
kudharauliwa huku wakijumuishwa kwenye kundi la wale wavunjifu wa maadili.
Kwa nini tuendeshwe na teknolojia badala ya sisi
tuiendeshe teknolojia ili tujitengenezea misingi mizuri ya maendeleo.
blog ni chombo kizuri ambacho kikitumika vizuri
kinaweza kuleta faida kadha wa kadha kwa mtumiaji. Inaweza kuwa kama sehemu
mojawapo ya kujiiingizia kipato, pia ni sehemu nzuri ya kufanyia mazoezi ya
uandishi haswa kwa wale wanaopenda kufanya uandishi.
Sasa kwa nini kijana ufungue blog na kuanza
kuchapisha picha na video za ngono? Unajichelewesha, kuna mengi unayoweza
kuyafanya kutumia blog yako na kufikia mafanikio.
Acha kupoteza muda kwa kuchapisha picha chafu
mtandaoni, igeuze blog yako kuwa chombo cha ukombozi.