Saturday, 27 June 2015

Kuhusu, Sepp Blatter ft Kujiuzulu FIFA

Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter amekariri kuwa hakujiuzulu kama rais wa shirikisho hilo.

Kiongozi huyo mswissi mwenye umri wa miaka 79 alikuwa amedhaniwa kujiondoa madarakani juni tarehe 2 kufuatia kashfa kubwa ya ufisadi ulaji rushwa na matumizi mabaya ya madaraka iliyokumba shirikisho lake lakini sasa anaonesha dalili za kubadili mtazamo huo.

Blatter ambaye ameiongoza FIFA kwa miaka 17 alikuwa ametangaza kuwa atajiondoa mbele ya kamati kuu ilikufanyike uchunguzi wa kina katika FIFA lakini sasa ameikumbusha jarida moja la uswisi BLICK kuwa yeye ndiye rais wa FIFA na kuwa aliweka hatima yake mikononi mwa kamati kuu ya shirikisho katika mkutano wa dharura.