Je ni kweli Ramos anaitumia Man U kuboreshewa mkataba Real Madrid?
Rio Ferdinand anaamini kwamba Sergio Ramos anaitumia Manchester United ili aboreshewe mkataba wake Real Madrid.
Manchester United wamekuwa wakihusishwa na kumchukua Sergio lakini hata hivyo Ferdinand aamini kabisa kama Man U watamchukua.
"Ramos kwenda Manchester United? Hilo haliwezi kutokea. Hawezi kwenda Manchester United," Ferdinand alisema kwenye mtandao wake.