Waziri mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu kama sehemu ya kuwajibika kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia suala zima la ferry iliyozama siku 11 zilizopita.
Chung Hong Won amesema kuwa kuendelea kusalia ofisini ni mzigo mkubwa kwake.
Bwana Chung alizomewa alipozitembelea familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara ya shule.
Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama. Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo. Via Bbcswahili