Tanzania inatarajiwa kuondoka
kwenye kundi la nchi masikini na
kuhamia kwenye kundi la nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akifungua kongamano linaloendelea hapa nchini.
Kongamano hilo ni njia mojawapo ya kuadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uliozaa nchi mpya ya Tanzania.
Kongamano hilo linakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabalozi, wataalamu na wafanyabiashara, ambapo
Profesa Muhongo alipata nafasi ya
kuwasilisha mada kuhusiana na fursa zilizopo katika sekta ya gesi, mafuta na madini.