Johannesburg: Askofu mkuu nchini Afrika kusini, Desmond Tutu amesema kuwa yuko na furaha sana Rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson mandela kuwa amekufa na wapigania uhuru wengine pia kwa kile alichodai wasingejisikia vizuri kushuhudi mababadiliko ya kimaendeleo yanayoenda taratibu mno nchini humo.
Tutu alikaririwa akisema, "ninafurahi sana watu hawa hawapo kushuhudia haya yanayotokea". Tutu alitoa maoni hayo alipofanya mahojiano kuhusu kitabu chake kipya anachotarajia kukitos karibuni.
Lakini kwa upande mwingine, mwenyekiti wa chama cha ANC, Gwede Mantashe alikaririwa akisema kuwa, "tatizo kubwa nchini humu ni kwamba kila mtu anamzungumzia Nelson Mandela, ila watu hao sio watendaji wazuri kama Mandela".
Askofu Desmond Tutu. Via Omgghana