Huyu jamaa ambaye hakuweza kutambulika kwa jina amepokea kichapo kitakatifu toka kwa wanakijiji wa kijiji cha Mbekenyera wilayani Ruangwa mkoani Lindi kwa kile kinachodaiwa kuwa amemuua kaka yake. Ripoti zinasema kuwa jamaa huyo alimuua kaka yake na kumwacha ndani ya nyumba yao na kukimbia kusikojulikana ndipo wanakijiji walipomtafuta na kumwangushia kipigo hicho.
(Picha na Octavian Nnunduma)