Tuesday, 22 April 2014

Kaiba mihogo ya Sh.500 kahukumiwa miaka 10 jela ila wengine wanaiba mabilioni wanaachwa

Yaw Nkrumah, 28, mkazi wa nchi ya Ghana amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na kazi ngumu kwa kosa la kuiba mihogo ya mkulima mwenzie. Alihukumiwa kifungo hicho baada ya hakimu kumkuta na hatia bwana Yaw ambaye mwanzoni kabla hajapelekwa mahakamani alimwomba aliyemuibia wayamalize ila alikataliewa. Inasemwa kuwa, mtuhumiwa alihoji kwa nini yeye ameiba mihogo ya 500 kahukumiwa miaka 10 jela na wengine wanaiba mabilioni wanaachwa!?