Mwanamke mmoja huko China aliamua kutengeneza sabuni kutumia maziwa yake mwenyewe baada ya mwanae wa kiume kugoma kunyonya.
Baada ya kutengeneza sabuni hizo aliitumia kumwogeshea mwanae na kupata matokeo mazuri kwa kumng'arisha mtoto wake.
Baadae mama huyo alizitengeneza za kutosha na kuamua kuziuza kwenye mitandao kama vile ebay, amazon na taobao ya China.
Imesemwa kuwa, kwa kutumia sabuni hizo za maziwa ya mama,unaweza kuondoa chunusi kwa haraka na ufanisi.
Baadhi ya sabuni zilizotengenezwa na mama huyo kutumia maziwa yake. Via Closeronline