Monday, 28 April 2014

Mtabiri asema ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea itaonekana Juni 12 mwaka huu

Ndege ya Malaysia MH370 itaonekana Juni 12 mwaka huu, mtabiri kiongozi wa dini alisema.

Kijana kiongozi wa dini ya kiislamu nchini Ghana, Shamu- na Ustaz Jibril, ametoa maono juu ya upotevu wa ndege ya Malaysia MH370 na kuzungumzia kilichokwamisha juhudi za kuitafuta.

Alisema  kuwa abiria wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wameshakufa.

Akizungumza na Daily Guide, alisema kuwa alioteshwa majina ya abiria wote waliokuwepo kwenye ndege hiyo, taarifa alizosema zilimjia kimiujiza.

Alitaja baadhi ya majina ya abiria waliokiwemo kama vile, Zhangke Jia, Woo-ping Yen, Shanbo Qin, Jingchin Zhang among na wengine.

Kuhusu rubani alisema kuwa, "alikuwa na ugomvi na mke wake muda mfupi kabla ya kurusha ndege hiyo, rafiki yake nae alitupwa jela siku kabla. Pia aliota anavamiwa na nyoka mkubwa hivyo alipokuwa akirusha ndege alifikiria kuhusu yote haya na kupoteza mwelekeo."

Hivyo alisema kuwa, "itaonekana siku 45 kutoka leo, (jumamosi iliyopita Aprili 16 2014). Alikazia kuwa, watafutaji wanatakiwa wawe makini siku ya tarehe Aprili 29 na Juni 6. Ilisemwa kuwa kama ndege haitapatikana siku tajwa basi haitapatikana tena.

Alimalizia kwa kusema kuwa yeye kama yeye amekariri kitabu cha kuran na alidai kuwa hajafundishwa na yeyote.

Via Daily Guide