Saturday, 19 April 2014

(Picha) Dada aliyepandikizwa UKE aeleza matumaini ya kupata watoto kupitia UKE huo na kujenga familia.

Itakumbukwa kuwa kwenye mfululizo wa habari zetu, vitendo blog iliwahi kukuletea taarifa kuhusu wanawake wanne waliofanikiwa kupandikizwa UKE uliotengenezwa maabara

Hivyo basi, huyu ni mmoja kati ya hao wanawake wanne ambao wanefanikiwa kupandikizwa UKE uliotengenezwa maabara ambaye hakutaja jina lake ambaye pia ni mkazi wa Mexico.

Dada huyo kwa matumaini makubwa sana alisema kuwa, anategemea siku moja atakuja kuwa na familia kupitia UKE huo aliopandikizwa.

Itakumbukwa pia, dada huyu alizaliwa bila UKE au UKE wake kuwa na matatizo hivyo kupandikizwa UKE uliotengenezwa maabara kutumia viini (cells) za mwanamke.

Via Daily mail