Monday, 28 April 2014

Muda mfupi uliopita: Gari ya kampuni ya Hood iliyokuwa imebeba abiria 55 yateketea kwa moto

Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Mbeya kuelekea Arusha na basi la kampuni ya Hood lenye namba T 173, wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuwaka moto na kuteketea.

Akizungumzia ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Orich Matei amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo jioni katika kijiji cha Kilolele mkoani Pwani.

Alisema kuwa ajali ilitokea baada ya kupasuka kw matairi ya mbele na kuanza kutoa cheche na ndipo dereva alipowataka abiria kushuka. Mizigo na vifaa vingine vimeteketea.

Via RadioOne