Watu 3 wahofiwa kupoteza maisha kwa kile kinachodaiwa kuwa walikula nyama ambayo ilikuwa na sumu huko Kakamega Kenya.
Inaaminika kuwa ng'ombe ambaye walikula nyama yake aliathirika na na ugonjwa wa Anthrax.
Ripoti zinasema kuwa jamaa hao waliamua kumchuna ng'ombe aliyekufa ambaye aliaminika kuwa na ugonjwa wa Anthrax na kula nyama yake.
Francis Shikokoti ni mmoja kati ya jamaa 3 waliokufa baada ya kula nyama hiyo huku wengine 2 hawakuweza kutambulika.
Watu wengine kadhaa wameripotiwa kuwa na hali mbaya na kupatwa na makwinyanzi kwenye ngozi zao waliyoyapata mara tu baada ya kula nyama hiyo.
Josephat Matikho ni daktari aliyekwenda eneo la tukio na kuthibitisha kuwa ng'ombe huyo alikufa na ugonjwa uliotajwa.