Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter nchini Uturuki wameripoti kuwa mtandao huo umefungwa.
Watumiaji wa twitter nchino humo walipokuwa wakijaribu kuingia kwenye tovuti ya www.twitter.com walikitana na kauli ya mamlaka ya mawasiliano iliyosema hatua za kiusalama.
Hii imetokea baada ya waziri mkuu nchini humo, Recep Tayyip Erdogan Kutoa tamko la kuufungia mtandao huo kwa kile kilichpdaiwa kuwa umetumika kutoa siri zake za rushwa.
"Sijali jumuiya za kimataifa zitasema nini kabisa, kila mtu ataona nguvu ya jamhuli ya uturuki," alisema Erdogan mapema alhamisi.
Aliyasema hayo baada ya watumiaji wa twitter kuchapisha machapisho yanayoonesha ushahidi unaomuhusisha waziri huyo na rushwa.