Snura asema atapunguza viuno
kwenye video zake, adai ataendeleza akiwa jukwaani.
Mwimbaji wa Bongo Flava ambaye pia ni muigizaji wa filamu za kitanzania, Snura amesema kuwa
amepunguza viuno kwenye video za nyimbo zake kutokana na kukosolewa na hata kutolewa kwenye baadhi ya vipengele vya KTMA.
Akiongea katika kipindi cha Redio, Snura ameeleza kuwa hata kabla BASATA hawajapiga marufuku ushiriki wa nyimbo zake kwenye kinyang’anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards alikuwa
ameshabadilika kwa kuwa tayari video yake ya ‘Nimevurugwa’ ilikuwa imefungiwa.
“Tayari mimi nilishabadilika kabla hata hatujafika huko kwenye Kili kwa sababu ilifungiwa muda kidogo kabla mambo ya Kili hayajaingia. Na wimbo wangu wa Ushaharibu nilikuwa nimeshafanya video pia. Wimbo wangu wa Ushaharibu ukitoka watu watajua ni jinsi gani
nimeweza ku-change.” Amesema Snura.