Suala la baadhi ya watu kuathiliwa na simu zao(smart phone) lipo na inawezekana ikawa wewe au kuna mtu unamfahamu aliyeathiliwa.
Dalili mojawapo kati ya hizi ni kuwa wewe umeathiliwa na smart phone
Moja, unapatwa na paniki na wasiwasi mkubwa sana unaposahau ulipoiweka simu yako na kuitafuta bila kuiona kwa dakika kama mbili.
Pili, unashindwa kufuatilia mazungumzo muhimu pindi unapokuwa unazungumza na mwenzako. Unawekeza utayali mkubwa sana kwenye smart phone badala ya mazingumzo. Pia unashindwa kufahamu kilichokuwa kinaendelea mwisho wa mazungumzo. Tatu, kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuchati na watu zaidi ya wanne kwenye 'whatsapp' au 'sms' kwa mkoupuo. Wengi wao hii wanayo, je wewe? Nne, wengi huwa wana ile hali ya ushapu wa kuangalia mara kwa mara kujua nani ametuma ujumbe na kuwa na mchecheto wa kujibu ndani ya muda. Tano, hii nayo wanayo wengi, unakuwa bored na disappointed unapoangalia simu yako na bila kutegemea hukuti notification yoyote.