Friday, 28 March 2014

Jamaa bado hawajachoka kuitafuta ndege ya Malaysia iliyopotea, waamia sehemu nyingine. Ebu twende hapa na vitendo ukapate kufahamu wanapoitafuta.

Maafisa wanaosaidia katika harakati za kuitafuta ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea majuma tatu yaliyopita,wametangaza kuwa wanabadilisha eneo la kuitafuta mabaki ya ndege hiyo.

Eneo hilo jipya litakuwa kilomita elfu moja mia moja kaskazini mashariki mwa kusini mwa bahari
hindi.

Mamlaka ya usalama wa baharini nchini Australia imesema kuwa hatua hiyo inatokana na taarifa muhimu na utafiti wa Malaysia pamoja na matokeo ya utafiti wa rada ya ndege hiyo iliyotoweka.

Ndege hiyo iliyotoweka March tarehe 8 ikiwa na abiria 239 sasa inadaiwa kwamba ilikuwa katika
mwendo wa kasi kinyume na ilivyokadiriwa na kwamba huenda iliishiwa na mafuta ghafla.

Meneja mkuu wa shirika la utafiti wa anga za juu ya Australia John Young, amesema utafiti mpya
unaonesha kuwa ndege hiyo ya MH370 ilikwea juu na kufululiza kwa kasi mno na hiyo inaweza
kuwa sababu ya mafuta ya ndege hiyo kumalizika haraka.

Eneo inakotafutwa ndege ya Malaysia Kutokana na hesabu hiyo mpya eneo la kutafutwa kwa ndege hiyo imehamishwa hadi umbali wa kilomita 1,850 Magharibi mwa Perth na itakuwa katika eneo lenye kilomita 319,000 mraba katika bahari Hindi .