Kufuatia kuwepo kwa kikundi cha watu au mtu fulani kusikika akisema ameagizwa kufikisha taarifa kwamba hawautaki muungano, bakozi Seif Ali Idd ambae ni makamu wa pili wa
rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar amezungumza na vyombo vya habari March 27
2014 na kusema.
"wanaosema Wazanzibari wote hawataki muungano bali wanataka
mkataba hii ni kauli potofu, alikutana nao wapi Wazanzibari hao wakasema hivyo? Wazanzibari
wako zaidi ya milioni moja na laki tatu.
"Alifanya nao wapi mkutano huo na kukubaliana kwamba uwepo muungano wa mkataba? ni
vyema angesema yeye na kundi lake ndio wanataka mkataba.
Balozi aliongeza kuwa, "kitendo cha baadhi ya viongozi hao wa kisiasa kuwataka Wazanzibari wanaofanya shughuli zao na kuishi Tanzania bara waache shughuli zao
na kurudi Znz, nia yao ni kuwatenganisha, kama haufahamu kiasili Wazanzibari wengi asili
yao ni Tanzania bara.
"Leo Zanzibar hakuna hata Mzanzibari mmoja atakaefatilia asili yake na kujikuta haihusu Tanzania bara hivyo suala la kuasisiwa kwa muungano mwaka April 1964 ilikua ni kurasimishwa tu lakini muungano huu ulikuepo
tayari miongoni mwa Wananchi wa pande hizi mbili, serikali ya Mapinduzi Zanzibar iko macho
na yeyote atakaejaribu kuleta fujo
atashughulikiwa kikamilifu."
Baada ya Waandishi kuhoji uwepo wa katiba mpya ya Zanzibar Balozi alijibu,
"Ni kweli Zanzibar ni nchi kwa sababu ni moja ya nchi zilizofanya muungano isipokua tofauti ni moja tu ambayo wengi hawaielewi, Zanzibar haina utaifa, Tanganyika na Zanzibar zote zimechukuliwa na Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania, kwani ukienda nchi za nje huwa unakuta ubalozi wa Znz? hapana haupo.
"Hili suala lisiwachanganye bure kwa sababu katiba ile imebadilishwa kutokana na
makubaliano ya kuingiza swala la serikali ya umoja wa kitaifa."