Thursday, 27 March 2014

Afisa wa JWTZ na hatia ya kughushi, kilichomkuta hiki hapa, hatari! Tusindikizane hapa na vitendo.

Mwanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Muhsin Kombo amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kughushi.

Hakimu Mkazi Waliarwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es.Salaam, alitoa hukumu hiyo jana baada ya
kupitia ushahidi wa mashahidi 19 na vielelezo vya upande wa Jamhuri pamoja na utetezi wa washitakiwa.

Kombo na mkewe Devotha Soko walikuwa wanakabiliwa na mashitaka sita ya kupanga njama, kughushi, kutoa taarifa za uongo na
kujipatia Sh milioni 100 kwa njia ya
udanganyifu.

Katika hukumu yake jana, Hakimu Lema alimuachia huru Devotha kwa kuwa upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake na Kombo alitiwa
hatiani kwa shitaka la kughushi.

Kombo ametiwa hatiani kwa mashitaka ya  kughushi muhtasari wa kikao kilichofanyika Machi 25 mwaka 2008 akionesha kuwa,
Devotha amechaguliwa na familia ya marehemu Awadh Ally kusimamia mirathi.

Katika mashitaka mengine ilidaiwa Mei 5 mwaka 2008 katika Mahakama ya Mwanzo Sinza, jijini Dar es Salaam, washitakiwa walitoa taarifa za uongo kwa Hakimu wa
Mahakama.

Inadaiwa walitoa taarifa kwamba Ally alifariki mwaka 1986 na kuacha watoto wawili, jambo lililosababisha hakimu huyo
kumteua Devotha kuwa msimamizi wa mirathi.

Aidha inadaiwa Januari 28 mwaka 2011, washitakiwa walijipatia Sh milioni 100 kutoka kwa Rukia Zidadu kwa madai ya kumuuzia nyumba yao iliyopo Kijitonyama
katika kiwanja namba 281 block 46.