Mkazi wa kijiji cha Mchinga Namba Moja wilayani Lindi mkoani humo, Mohammedi Maji (71) anadaiwa kumbaka mtoto wa kambo wa miaka 7.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Foka Diniya alisema tukio hilo lilitokea saa 5.00 usiku nyumbani kwa mtuhumiwa, ambaye alikuwa anaishi na mkewe, ambaye ndiye mwenye mtoto huyo wa kike aliyezaa na mume mwingine.
Alisema kuwa mtoto huyo (jina
linahifadhiwa), hajaanza shule na yuko nyumbani.
Alisema taarifa zilifikishwa polisi na
mtuhumiwa alikamatwa na wakati wowote atafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma hizo.
Kamanda Diniya alisema ofisi ya
mwanasheria mkuu wa serikali, ilitoa maagizo kwa polisi, wafanye uchunguzi zaidi na mtuhumiwa alipewa dhamana.