Mke mtarajiwa wa Kanye west, bibie Kim Kardashian ametajwa kwenye orodha ndefu ya wanawake maarufu ambao mume wa Mariah Carey, Nick Cannon amepenzika nao.
Nick Cannon aliitaja orodha hiyo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo fulani cha redio na alisema anakumbuka mbali sana akivuta picha ya uhusiano huo aliowahi kuwa nao na Kim.
Aliwataja wanawake wengine kuwa ni Christina Milian, Nicole Scherzinger and Selita Ebanks na kwa sasa yupo na Mariah Carey.
Sasa sijui mzee Kanye atajiskia akilisikia hili la mkewe mtarajiwa kuwahi kuwashwa moto na jamaa huyo.
Mariah Carey nae je!?
Nick Cannon na mkewe Mariah Carey