Friday, 28 February 2014

Kweli huwezi kosa vyote! Msomaji wa vitendo blog, ulishawahi kumuona mtoto kama huyu mwenye ulemavu wa ngozi, ulemavu wa mikono na ulemavu wa macho pia, lakini ana uwezo wa kuchora!? Fuatilia hapa na vitendo ukamuone kijana huyo.

Ni Emmanuel Festo (12) mtoto mwenye ulemavu wa ngozi. Pia ni ulemavu wa mikono ambayo aliipoteza baada ya kuvamiwa na kukatwa viganja vyake mwaka 2006 mkoani Kagera akionyesha uwezo wake alionao wa kuchora. Mtoto huyu pia ana matatizo ya kutoona vizuri kutokana na maumbile yake.