Kumuhimiza mtoto kuhusu kujisomea pindi arudipo nyumbani toka shule ni suala ambalo mzazi au mlezi unapaswa kuwa wimbo wake wa kila siku kwa mtoto.
Hii itamjengea mtoto tabia na utamaduni wa kupenda kujisomea na kujiwekea mazingira mazuri katika ufaulu wa masomo yake, hivyo mzazi au mlezi anashauriwa kumuhimiza mtoto kujisomea pindi anaporudi nyumbani.
AMKA mzazi, AMKA mlezi, mjengee mtoto mazingira ya kufanya vizuri katika masomo yake kwa kumuhimiza kujisomea.