Thursday, 27 February 2014

Benki ya dunia imegailisha kuisaidia Uganda!? Imerudisha kitita cha dola milioni 90 mfukoni!? Fuatilia hapa na vitendo kufahamu zaidi.

Benki ya dunia imegailisha mpango wake wa kutoa mkopo wa dala milioni 90 kwa nchi ya Uganda kwa kile kinachodaiwa kuwa ni sababu ya sheria yake ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja.

Maafisa wa benki ya dunia walisema kuwa walikuwa wanataka kuhakikisha miradi iliyokusudiwa msaada huo utumike haitaathiriwa na uwepo wa sheria mpya ya kuzuia ushoga.

Msaada huo ambao ulilenga kusaidia kuinua huduma za kiafya nchini Uganda umeonekana kuingia doa kutokana uwepo wa sheria hiyo.

Sheria iliyopitishwa jumatatu inayotoa adhabu kali kwa wake wanaokutwa na hatia ya juhohusisha vitendo vya  ushoga.

Kwenye picha ni secta mojawapo ambayo ni ya afya ambayo msaada wa benki ya dunia ulilenga kusaidia.