Madereva na makonda wa daladala siku zote huwa ni watu wenye haraka mno wawapo katika sehemu zao za kazi haswa wakati wa kushusha abiria na wakati wa kupakia pia.
Haraka walizonazo madereva na makonda wa daladala zinawatengenezea abiria mazingira hatari ya kupata ajali hivyo madereva wanashauriwa kusimamisha gari kwanza ili abiria aweze kupanda ama kushuka kwa usalama.
AMKA dereva AMKA kondakta, ili kuepuka ajali zisizo za lazima kama niliyoishuhudia juzi maeneo ya Kariakoo ya abiria kupoteza fahamu baada ya kutaka kudandia daladala iliyokuwa kwenye mwendo na kukosea kudandia na kujikuta akidondoka vibaya.