Barcelona waripotiwa kwamba wanataka kumsajili kiungo mlinzi wa Manchester United Daley Blind, kwa mujibu wa Sportreports kupitia Daily Mail.
Tetesi zilizozagaa ulimwengu wa soka katika siku za hivi karibuni zilidai kwamba meneja mpya waManchester United Jose Mourinho ana nia ya kumuuza Mholanzi, wakati mabingwa wa La Liga wamejipanga kutoa £14m kumnunua mchezaji.
Aidha, mwenye umri wa miaka 26 amesisitiza kuwa atafanya kazi kwa bidii chini ya ukufunzi wa Mourinho kupigania nafasi yake ndani ya Old Trafford huku kukiwa na uvumi unaomhusisha na kuiondoka klabu.
Messi
Blind