Mamlaka nchini Pakistan imepiga marufuku matangazo ya bidhaa za kupanga uzazi.
Bodi inayodhibiti matangazo ya redio na runinga imeagiza vituo vya utangazaji kuondoa matangazo hayo kutokana na lalama za raia, kuwa yanawafanya watoto kuwa wenye kutaka kujua sana.
Mwaka jana tangazo la aina moja ya kondomu lilipigwa marufuku kwakuwa potovu, japo matangazo ya dawa za kupanga uzazi huwa nadra sana katika taifa hilo la kihafidhina.
Pakistan inaorodheshwa ya sita duniani kwa idadi kubwa ya watu.Umoja wa Mataifa unasema thuluthimoja ya raia wa taifa hilo hawafikiwina huduma za kupanga uzazi.