Monday, 30 May 2016

Amini usiami, lazima ushangae ukiijua sababu iliyozalisha bifu nzito kati ya Shilole na Vee Money

Ule usemi usemao ukitaka kumtawala mjinga basi cheza na fikra zake umetimia baada ya madada hawa wawili kuzitawala fikra za watanzania waliowengi kwa kuwaaminisha kwamba kuna bifu nzito baina ya madiva hao.

Mchezo uliokuwa ukiendelea ambao uliokuwa na sura yenye mwonekano wa bifu nzito uliokuwa ukichezwa na Shilole pamoja na Vee Money ilikuwa ni danganya toto ili mwisho wa siku waje watimize lengo lao.

Shishi na Vee wamelithibitisha ilo kwenye shoo yao iliyofanyika jana 29 mei baada ya wao wenyewe kufunguka na kuwaelezea mashabiki zao kuwa haikuwa bifu bali ilikuwa ni kutafuta kiki ya kubusti shoo yao na pia ilikuwa kuwakumbusha watu kuwa wasiamini kila wanachokiona mtandaoni.

“Kiukweli haukuwa ugomvi bali tulijaribu kuwaonesha watu kuwa usiamini kila unachokiona kwenye mitandao, namuheshimu sana Shilole katika kazizake, lakini baada ya sisi kufanya vile watu walionekana kama wanataka kuona sisi tukigombana," Vee Money alisema.