Friday, 2 May 2014

(Mpya) Hatimaye Chelsea wamnasa Diego Costa

Mchezaji wa timu ya Atletico Madrid, Diego Costa, amekubali kusaini mkataba wa kwenda kuichezea klabu ya chelsea.

Kwa sasa Chelsea wamempata mtu ambaye walikuwa wakimfukuzia kwa miezi kadhaa baada ya Costa kuridhia kusaini.

Costa ambaye aliitandaka Chelsea kwenye mechi ya Klabu bingwa Ulaya wiki hii anasemwa kuwa ndiye mchezaji wa kwanza aliyepewa kipaumbele cha kusajiliwa na bosi wa klabu ya Chelsea mzee mbwatukaji.

Ripoti zinasema kuwa Klabu ya chelsea imefungasha kitita cha £32million.

Mourinho akimkodolea Costa Costa akipiga penati kwenye mechi dhidi ya Chelsea. Via Metro