Droo ya kuamua nani anapambana na nani kwenye ligi ya mabingwa Ulaya imechezeshwa leo na droo imetoka kama ifuatavyo.
Mechi za kwanza zitapigwa jumanne, Aprili 22 kati ya Atletico Madrid na Chelsea na jumatano, Aprili 23 kati ya Real Madrid na Bayern Munich
Mechi za marudiano zitapigwa wiki itakayofuata baada ya wiki ya mechi ya kwanza, zitachezwa Jumanne, Aprili 29 kati ys Real Madrid na Bayern Munich, na Jumatano, Aprili 30 kati ya Atletico Madrid na Chelsea.
Na mechi ya mwisho ya kufunga mashindano itapigwa huko Lisbon Mei 24.