Mwanamke mmoja wa kichina amejikuta katika majuto baada ya kukuta maziwa yake aliyoyapandikiza mwaka 2002 yamesogea, moja likiwa mgongoni na lingine tumboni.
Aliamua kupandikiza maziwa hayo ili kumvutia mume wake aliyekuwa anamdanganya na mwanamke mwingine.
Tian Hui, 39, zaidi ya miaka 10 tangu afanye upasuaji lakini alikuwa akiona maziwa hayo yanasogea toka upande mmoja kwenda sehemu nyingine ambako ni mgongoni na tumboni.
Tian alikuwa akijaribu kuyasukuma yarudi yalipotakiwa kubaki ila bado jitihada zake hazikuweza kufanikiwa.
Tian mkazi wa Guangzhou huko china alihisi angekuwa na ndoa yenye furaha kwa kumridhisha mumewe na maziwa mchongoko ambayo alisema mumewe huyo alikuwa anayafuata kwa mwanamke mwingine.
Ziwa lililosogea mgongoni Ziwa lililosogea tumboni