Wednesday, 5 March 2014

Msomaji wa vitendo blog ningependa nikushirikishe hili lilitokea kwenye msiba fulani saa kadhaa zilizopita wakati wa harakati za kutafuta mahali pa kuchimba kabuli.

Ilikuwa kwenye makabuli ya kwa Jimmy maeneo ya machimbo mwisho wa lami jijini Dar.

Kulikuwa na shida kupata eneo la kuchimba kabuli, eneo lililopatikana lilizungukwa na makabuli, yaani sehemu yenyewe ilikuwa imetumika tayari hivyo chini kulikuwa na mfu.

Pili upande wa kulia kulikuwa na kabuli, kushoto nako, mbele na nyuma nako kulikuwa na makabuli  na hali hii kusababisha kabuli kubomokea kila likichimbwa.

Mwishoni ikabidi kuchukua matofali na kujengea ili udongo usibomokee.

"Kujaa kwa eneo hili ndio chanzo cha haya yote", mzikaji mmoja alisema.