Tuesday, 18 March 2014

Mourinho ammwagia sifa Didier Drogba. Fuatana na vitendo kupata mengi zaidi.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anaamini kuwa gwiji wa soka Didier Drogba bado ni nyota kwenye safu ya washambuliaji bora zaidi duniani.

Drogba anayesakata soka yake na klabu ya Galatasaray na ambaye aliondoka Stamford Bridge Juni mwaka 2012, leo anarejea kwa
mkondo wa pili wa vilabu vilivyosalia katika kombe la klabu Bingwa Ulaya kufuzu michunao
hiyo.

Ikiwa Drogba ataingiza bao huenda
asisherehekee uwanjani Stamford Bridge Mourinho alisema Drogba angali na makali aliyokuwa nayo alipokuwa miaka 26 , na hakuna
anayeweza kuwa katika hali hiyo akiwa na umri wa miaka 36.

Lakini ni mshambulizi hodari sana.
Drogba amesema huenda hatasherehekea ikiwa ataingiza bao dhidi ya wachezaji wenzake wa
zamani.

Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast aliingiza mabao 157 katika mechi 342 wakati alipokuwa anachezea Chelsea kwa miaka minane.

Mourinho, aliyemsajili Drogba katika klabu ya Chelsea kutoka Marseille mnamo mwaka 2004,
alishangiliwa sana aliporejea katika klabu hiyo mwezi Agosti mwaka jana baada ya kuwa nje kwa
karibu miaka sita.

Anatumai kuwa Drogba atang'aa katika mechi ya leo usiku. Chelsea itakuwa klabu ya kwanza, kufika robo fainali ya michuano hiyo ikiwa watashinda mechi ya leo usiku dhidi ya Galatasaray na duru zinasema kuwa Mourinho yuko ngangari