Thursday, 20 March 2014

Maajabu haya, mtoto aliyezaliwa wakati ajali inatokea na kuwa mzima. Ebu fuatana na vitendo hapa upate kufahamu maajabu haya yalivyotokea.

Mtoto mmoja amenusurika kifo baada ya kuzaliwa wakati ajali iliyohusisha kugongana roli na pikipiki inatokea ambayo ilimsababishia mama yake kifo, na mara baada ya ajali mtoto huyo alishazaliwa.

Hii ilitokea pale wakati mama huyo baada ya kusikia uchungu na kupakiwa kwenye pikipiki na baba wa mtoto huyo kuelekea hospitali kujifungua.

Wakati wapo njiani, pikipiki yao iligongana na roli tukia lililomtupa pembeni mama wa mtoto huku akiendelea kujifungua.

Mtoto alikutwa umbali wa mita 4 tu kutoka eneo alilokuwepo mama yake, alieleza askari aliyeshuhudia tukio hilo huko China.

Dereva wa pikipiki ambaye ni baba wa mtoto huyo alifariki dunia papo hapo.