Akizungumzia historia ya maisha yake kwenye kituo fulani cha redio leo asubuhi Ney alieleza kuwa.
Kuhusu kufukuzwa
Ney alisema kwamba, baada ya mama yake mzazi kugundua Ney amejiingiza kwenye kazi ya muziki, mama yake hakuridhika na kitendo cha mwanae kujihusisha na muziki.
Hivyo Ney aliambiwa achague moja kati ya kuhama nyumbani na kwenda anakokujua au kufuata aliyoyataka mama ikiwa ni kukacha muziki. Ney alisema yeye alichagua kuhichanganya na kufanya muziki.
Kuhusu kutia mimba
Ney alisema kuwa wakati yupo kidato cha kwanza alijikuta akimpa ujauzito mwanafunzi mwenzake ( mtoto wa kihindi) aliyekuwa na uhusiano nae na kufanikiwa kuzaa nae.
Jambo hilo lilimsababisha Ney aachane na uhuni aliosema alikuwa nao haswa wa kuvuta bangi aliyokuwa akinunuliwa na mtoto huyo wa kihindi, hii yote ilikuwa ni kwa vile alikuwa anatarajia kuitwa baba.