Sunday, 9 February 2014

WAZAZI WAMUUA MTOTO KWA KUMLAZIMISHA KUNYWA SODA.

Wazazi wamejikuta wakimsababishia mtoto wao, Alexa Linboom mwenye umri wa miaka 5 kifo kwa kumlazimisha kunywa soda ya zabibu kupita kiasi.

Taarifa zinaeleza kuwa, Alexa alilazimishwa kunywa soda hiyo kama adhabu kwa kosa la kuchukua soda ya mama yake wa  kambo.

Wazazi hao wamesomewa shitaka lao mahakamani jana baada ya uchunguzi kufanyika miaka miwili iliyopita huko Tennessee.

Chanzo, CNN.