Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Agnes Daud mkazi wa wilayani Chunya mkoani Mbeya anasadikiwa kuuawa na mumewe kwa kukatwa koo na mumewe, Thomas Msukuma.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi alieleza kwamba, Agnes Daud aliuawa na mumewe Thomas Msukuma na kuwa mwili wake ulikutwa umekatwa koo na kutelekezwa kwenye kibanda walimokuwa wakiishi.
Alisema kwamba sababu ya mauaji hayo ni chuki za mapenzi.
Chanzo, Nipashe.