Wafanyabiashara wa mikoa ya Ruvuma na Musoma wameingia kwenye mgomo leo kwa kile wanachodai ni kugomea matumizi ya mashine maalumu za elekroniki za kutolea stakabadhi (risiti).
Mgomo huo katika mikoa hiyo umewahusisha wafanyabiashara wa aina zote wakiwemo na wale wenye biashara ndogondogo ambao hawatumii mashine hizo.
Wananchi wa mikoa hiyo wanaotoka maeneo mbalimbali kwenda kupata huduma za kijamii mijini wamelalamikia tatizo hilo kuwa ni kero kubwa inayohitaji ufumbuzi wa haraka.
Chanzo, Radio one.