Waswahili wanamsemo wao usemao "uchungu wa mwana aujuae mzazi", usemi huu kweli unaendana na yale yanayotokea kwenye jamii yetu. Akina mama wengi upata uchungu na kujiskia vibaya pindi wanapoona vijana wao wanaenda kinyume na maadili.
Siku moja nilikuwa nimetulia nyumbani, dakika kadhaa baadae nikamsikia mama fulani ambaye ni jirani yangu maeneo fulani jijini Dar akilalamikia tabia ya mwanae wa kike ya kujirahisisha kwa wanaume.
Nilimsikia akiitamka sentensi hii ambayo kiukweli ilionesha jinsi gani mama huyo alichukia, alisema, "wakikunyegesha tu na wewe unanyegeka", kauli hii inaonesha jinsi gani mama huyo alikerwa na tabia ya mwanae kujirahisisha.
Chanzo cha mama huyo kuanza kuropoka haya yote ni kwamba mama huyo alimsikia mwanae mara kadhaa akizungumza na wanaume kwenye simu na kuitikia lolote alilokuwa akiambiwa na vijana huo.
Aliendelea kuskika akilalamika kwa kusema kwamba hiyo si mara yake ya kwanza kujirahisisha kwa wanaume na kwa tabia yake hiyo thamani yake inapotea licha ya uzuri alionao.
Mama mzazi akiskika analalamika kiasi hiki basi ujue yamemgusa kama alivyokuswa jirani yangu huyu.
Mara kwa mara wazazi wengi aswa akina mama, wamekuwa wakilalamikia tabia chafu za watoto wao ambazo zimekuwa zikiwaumiza kwa kiasi kikubwa.