Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mmoja kati ya wafuasi wa kikundi hatari cha mbwa mwitu kinachojishughulisha na uporaji na ubakaji ameuawa na kikatili na wananchi wenye hasira kali maeneo ya mbagara leo mchana.
Matukio ya kuwaangamiza wanakikundi wa mbwa mwitu yanazidi kushika kasi kwa kile kinachodaiwa na wananchi kwamba wamechoshwa na vitendo vyao.
Tukio kama hili lilitokea maeneo ya kijiwe samri bombom ambako vijana watatu walioshukiwa kuwa ni wanakikundi wa kundi hilo walishambuliwa mpaka kufa na wananchi wenye hasira kali.
Vitendo vya ualifu wa kupora na kubaka jijini dar vinavyofanywa na vijana wa aina hii limekuwa ni tatizo sugu ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka sana.