Friday, 31 January 2014

MAMA AMTENGENEZEA MWANAE TABIA YA KULA KINYESI.

Inaaminika kwamba mama ni mtu anayebeba asilimia kubwa katika familia katika kuitengeneza tabia ya mtoto tangu anapozalia hadi anapofikia umri wa kujielewa, hivyo inashauriwa kwamba mama anapaswa kuwa makini juu ya kuilinda tabia ya mtoto.

Mama mmoja mkazi wa Kiwalani bom bom jijini Dar es Salaam amajikuta akimtengenezea mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja tabia ya kula chochote akionacho hadi kufikia kula kinyesi chake pindi anapotengwa kwa lengo la kujisaidia.

Mama wa mtoto huyo amekili mtoto wake kuwa na tabia hiyo na kusema kwamba mtoto wake amekuwa akifanya hivyo tangu siku nyingi.

Baba wa mtoto wa mtoto huyo alisema kwamba tabia ya mwanae kula kinyesi imechangiwa na mama yake kwani umpa vyakula mara kwa mara na bila mpangiliempangilie bila kujali mtoto ameshiba ama ajashiba.

Baba huyo aliongezea kwa kusema mama mtoto anakosa umakini na mwanae kwani yeye kama mama anapaswa amuangalie mwanae muda wote kwa kuwa bado ni mdogo.

Umakini wa akina mama kwa watoto wao ni jambo la muhimu sana, uangalizi wa karibu utamsaidia mtoto kuepukana na hatari zinazoweza kumuathiri mtoto kiafya kama hii ya kula kinyesi ambayo ni hatari kwa afya yake.