Thursday, 30 January 2014

Bodaboda haraka zimezidi barabarani, Ebu fuatilia hapa upate kufahamu zaidi na vitendo blog.

Imekuwa ni kama destuli kwa madereva wa pikipiki marufu kama bodaboda ususani katika jiji la Dar es salaam kuwa watu wenye haraka sana wawapo barabarani.

Imekuwa ikishuhudiwa kwenye makutano mengi ya barabara jijini wakiwa na haraka ya kukatisha kwenda upande mwingine bila kujali wameruhusiwa ama la, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za barabarani.

Hivi tuseme hawana elimu juu ya sheria na matumizi ya alama za barabarani? Kama jibu ni ndio, kwa nini wanakuwa hivi? Kama jibu ni hapana, kwa nini wanaruhusiwa kuingia barabarani wakati hawafahamu ipasavyo sheria na alama za barabarani!.

Tatizo la kukatisha kwenye makutano ya barabara  bila kuruhusiwa ni hatari, kwa maneno mengine inahatarisha usalama wao maana kuna uwezekano mkubwa sana wa kutokea kwa ajali ambazo zinaweza kupelekea vifo.

Kumekuwa na ajali nyingi sana za pikipiki ambazo nyingi kati ya hizo zimeripotiwa kusababishwa na kukosekana kwa umakini unaochangiwa na kutozifahamu sheria za barabarani.

Kwenye alama za pundamilia kwa mujibu wa sheria za barabarani ni sehemu ambayo waenda kwa miguu wanapaswa kuitumia kuvuka kuelekea upande wa pili lakini alama hizi kwa madereva bodaboda ni kama sehemu za kawaida.

Madereva hao wanashindwa kuheshimu alama hizo kwa kuwaachia waenda kwa miguu nafasi ya kuvuka pindi wanapotaka kuvuka kwa sababu ya haraka zao.

Kwa nini uwakatili waenda kwa miguu haki yao ya msingi ya kutumia barabara haswa kwenye vivuko mahususi kwa ajili yao? Watembea kwa miguu nao wana haki ya kutumia barabara pia.

Nyie madereva wa bodaboda punguzeni haraka muwapo barabarani na kama haraka hii ikipunguzwa basi hata matatizo mengine yanaweza kuepukika.