Monday, 6 June 2016

Mwana FA afunga pingu za maisha, ndoa yahudhuliwa na mastaa kibao

Baada ya Mwana FA kutuambia bado yupo yupo sana kwenye maisha ya kibachela sasa ameamua kuachana na hayo na kuamua kufunga pingu za maisha.

Rapa Mwana FA amefunga ndoa Jumapili hii ‘June 5 2016’ na mchumba wake Helga ambaye pia na mama wa mtoto wake.

Ndoa hiyo ya kiislamu imehudhuriwa na ndugu na marafiki zake wa karibu akiwemo AY, Hermy B, Ommy Dimpoz,Sallam, Dully Sykes, Alberto Msando na wengine wachache.