Katika soka tunazoea kuona wachezaji wakiwabusu wake zao au marafiki wa kike lakini lililo kinyume na kawaida kuona jambo hilo likitokea kati ya wachezaji wenyewe. Hebu tuangalie baadhi ya nyakati hizo za kiuwendawazimu.
4.Busu la Messi na Alba
Labda watu wengi hawakuweza kutambua jambo hili lakini kamera ziliweza kunasa tukio. Alaba hakuweza kuamini kama bao la Messi zuri. Alizimia kiakili na mara kwa mara akampiga busu mshambuliaji huyu. Messi naye alionekana kama amezimia wakati wa tendo. Wakati mwingine soka yaweza kuwa tendo la kimapenzi.
3.Busu la Debuchy na Giroud
Debuchy alitoa pasi saidizi kwa mwenzake wa Arsenal Olivier Giroud na mshambuliaji mwenyewe hakuwa na ajizi kufunga bao kwa timu ya taifa ya Ufaransa. Beki alimshika mikononi mwake mshambuliaji huyu na kumfanyia jambo lisilodhaniwa. Kama ilikuwa namna ya kushangilia bao au kauli yake binafsi hatuelewi kamwe. Kinachofahamika ni kwamba busu hili lilijulikana kote nchini Ufaransa.
2.Busu la Gerrard na Alonso
Kwa uhakika hili lilikuwa tukio la uzulufu. Liverpool waliweza kupata ushindi wa ajabu katika Ligi ya Mabingwa walipotwaa taji hilo mnamo 2005.
Walikuwa wamefungwa mabao 3-0 na AC Milan lakini wakatoka nyuma wakaweza kukomboa kisha wakapata ushindi kwa mikwaju ya penati. Lakini jinsi nahodha Steven Gerrard na kiungo mwenzake Xabi Alonso walivyochagua kusherehekea ushindi huo vilionekana namna nyingine. Uzulufu wa Instanbul 2005.
1.Busu la Gary Neville na Paul Scholes
Unapotazama tendo lenyewe utadhani kwamba wote walikuwa tayari kulitekeleza. Kwa matazamio ya mtu mara kwa mara inaonekana kama jambo lisilo la kawaida. Huwezi pata taswila yake. Hili lilikuwa jambo kali la kiuwendawazimu kati ya malegendi wawili wa Manchester United. Naamini hadi sasa bado hawawezi kutambua jinsi vilivyofanyika.