Polisi mkoani Ruvuma inachunguza kifo cha mwanafunzi wa darasa la sita, Gloria Mrope (11) anayedaiwa kujinyonga.
Gloria ulikutwa ukining’inia kwenye mti nje ya nyumba ya wazazi wake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji alisemamwanafunzi huyo alikuwa akisoma Shule ya Msingi Mashujaa iliyopo Mahenge, Songea.
Alisema baada ya mwili wa Gloria kugundulika, uongozi wa Serikali ya mtaa na Kituo Kikuu cha Polisi cha mjini Songea ulipata taarifa zatukio hilo.
Alisema taarifa za awali zinadai hakukuwa na tatizo lolote kwenye familia kabla ya kifo hicho kutokea.